Monday, October 19, 2015

MAHAFALI UROKI SEKONDARI TAREHE


MAHAFALI UROKI SEKONDARI TAREHE 17 OCTOBER 2015

Siku hii ilithibitisha ule usemi wa Kiswahili kuwa siku njema huonekana asubuhi.

Wanafunzi wote walikua nadhifu na wenye haiba ya kisomi wengi wao wakiwa wamevalia sare mpya huku nyuso zao zikiakisi mwanga wa jua kwa tabasamu ambalo ni nadra sana kuliona shuleni na hasa shule za Tanzania. Hili lilikuwa jibu tosha kwa wale waliokuwa wakiuliza shule hii ina tofauti gani kubwa na shule nyingine? Mbona wazazi wengi wana watoto zaidi ya mmoja katika shule hii?

Baada ya ibada iliyoongozwa na mchungaji wa kituo (Chaplain) Mch Okuli Nkya, waafunzi na jumuiya nzima walikuwa na mapumziko mafupi ya kunywa chai nzito kwa wote.

Mapumziko yalimalizika baada ya nusu saa hivi na ndipo Maandamano ya kuingia ukumbinni yalipoanza kwa vishindo vya kwaito la nguvu.

Ndani ya ukumbi kelele za shangwe zilisikika kwa wale wanafunzi wangojezi ambao hawakuingia kwenye msafara huu, kelele zao zilikuwa kama kelele za maji mengi mfano wa yale ya maanguko ya maji ya Victoria kule Zimbabwe (Victoria Falls)

Mkuu wa shule Mwl Joseph Shahidi alionekana mwenye furaha  sana akitembea imara mithili ya askari tena wale wa mkoloni KAR, huku mkononi akiwa amebeba simu yake Smart Phone na bahasha yenye risala aliyomuandalia mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Hai.




Walimu na watumishi wengine nao walivalia vizuri sana. Jikoni muda wote kulikuwa na pilika pilika za kuandaa mahanjumati na kwa kuwa ukumbi haukua mbali sana na jikoni basi ungeweza kukisia aina za vyakula vilivyokuwa vinaandaliwa na hata kiasi cha mishikaki iliyokuwa imebanikwa jikoni.

Waandishi wa habari nao hawakuwa nyuma kuchukua matukio. Kwa kweli siku hii ilionekana ya kipekeee sana na yenye baraka zake nyingi sana.




Chapisho linalofuata litaelezea kinagaubaga ratiba nzima ya siku hiyo na tathmini ya wageni waliohudhuria. Hapa utweza kuona pia video na picha mnato nyingi kadri inavyowezeka.
Aidha kiamabatanisho cha risala zote na hotuba zote zilizotolewa siku hiyo zitajumuishwa.

Utapata nafasi ya kuwaona wahitimu wote na walimu baadhi waliokuwepo

Kwa sasa tuishie hapa











No comments: