Monday, October 19, 2015

MAHAFALI KIDATO CHA NNE 2015
Siku ilianza kwa Bashasha na msisimuko mkubwa sana.
Wanafunzi wakiwa wamevalia Sare zao safi zilizolandanda kabisa na haiba ya uanafunzi miongoni mwazo zikiwa mpya toka dukani huku zikinukia marashi ya kupendeza, waliianza siku kwa shukrani kwa Muumba wao katika ibada iliyoongozwa na Mchungaji wa Shule (Chaplain) Rev Okuli Nkya.

Ilipofika muda wa saa tatu hivi, wanafunzi na watumishi walijumuika kwa Chai nzuri ili kukoleza furaha ya siku.

Mara baada ya chai ndipo shangwe na nderemo zilipovumva ukumbini mfano wa maanguko ya maji kule Victoria (Victoria Falls) kule Zimbabwe zikipambwa na nyimbo na miruko ya Kwaito. Kidato cha nne walijipanda msururu mrefu uliomeremeta na huku wakicheza kwaito kwa nguvu zao zote wakiingia kwa maandamano ukumbini. Kwa nyuma watumishi na wageni wote walijiunga kwa mbwembwe na makofi.



Mkuu wa shule Mwl Joseph Shahidi alikuwa muda wote akitabasamu na mkononi akibeba bahasha yenye risala aliyomwandalia mgeni Rasmi. Miongoni mwa wageni waliokuwako ni Mzazi rasmi Mwl Philipo Kiula na wajumbe kadhaa wa Bodi ya shule.

Katika mada zitakazofuata tutaambatanisha video na nyimbo mbali mbali zilizoipamba siku hiyo

No comments: